Tuesday, 8 April 2014

Tibaijuka Awakumbuka waathirika wa Mvua Wilayani Muleba


 
Waziri Anna Tibaijuka


Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Pofesa .ANNA K. TIBAIJUKA {MB} Muleba kaskazini, amewatembelea wananchi waliopatwa na gharika ya mvua iliyonyesha tarehe 28march2014 na kuwapa pole kwa maafa yaliyo wakuta.
 Akiwa katika kijiji hicho yeye mwenyewe binafsi ameweza kuwapatia waathirika wa mvua msaada wa kiasi cha tani moja na nusu ya maharage yenye gharama ya tsh.1,500,000/=. Na kufafanua kuwa tani moja ni kwa ajili ya wananchi wa kijiji cha Bulembo na robo tani igawiwe kwa wananchi wa kijiji cha Mafumbo.
 Aidha Pr.ANNA amewahusia wananchi na kamati ya maafa ya kijiji kwa ujumla kuwa misaada inayoletwa kijijini hapo haimbagui mtu yeyote na igawiwe kwa usawa bila kujali itikadi za vyama wala dini kwa wahusika.  
 Akikabidhi msaada huo kwa wananchi waliohudhulia amesema kuwa yeye ameguswa sana na janga hili na kusema japo alikuwa nje ya nchi hayuko mbali nao, amewaahidi wananchi hao kuwa kwa nafasi aliyonayo serikalini atahakikisha misaada ya kiserikali inatolewa na kuletwa kwa wahusika.
 Pia kawapa salamu kutoka kwa mbunge wao ndg Mwijage kuwa japo yuko bungeni lakini yuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu. Sanjari na hayo Pr.ANNA amewapatia wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kiasi cha shilingi 250,000/= kwa kukarabati ya ofisi ya chama hicho iliyoezuliwa na mvua katika kijiji hicho. 

Imetumwa na ALLAWI BASHIRU…………….

No comments:

Post a Comment