![]() |
Mwenyekiti wa KDCU, Ndg. Prosper Murungi |
Kyerwa - Kagera
Chama cha msingi cha ushirika cha Kamuli wilayani Kyelwa Mkoani kagera kimetenga
fedha zaidi ya shilingi laki tano kwa ajili ya kupanda miche ya miti mbalimbali
ili kuboresha mazingira.
Wakati
mvua zikiwa zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali wilayani Kyerwa uongozi
wa chama cha msingi cha ushirika kamuli kikiongozwa na mwenyekiti wake Prosper
Murungi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha wilaya za
Kyerwa na Karagwe KDCU LTD, walitenga
kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya kupanda miti ya aina mbali mbali
katika ardhi ya chama hicho kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.
Murungi
amewaelekeza wakulima katika ushirika huo kuwa njia pekee ya kuwa na mafanikio
ni kujiunga na ushirika baadae kukopa kwa malengo na kurejesha kwa busara.
Mkutano
mkuu katika chama cha msingi cha Kamuli ambao ni kupanga bajeti ya mwaka
2014/2015 uliofanyika hivi karibuni umeridhia mapendekezo hayo na kufikia sasa mchakato wa upandaji miti
unaendelea.
Baadhi
ya wanachama walishukuru kuwepo kwa mapendekezo hayo ya kununua miche na
kueleza kwamba mazingira yanapopandwa miti huvutia lakini pia miti huvuta mvua
katika eneo ambapo inakuwa imepandwa.
Vyama
vya msingi vya ushirika wilayani Kyerwa vinajihusisha na ununuzi wa zao la
kahawa ambalo ni zao la biashara katika wilaya za Kyerwa na Karagwe.
No comments:
Post a Comment