Tuesday, 8 April 2014

Karagwe yaendelea kuwa na upungufu wa walimu

Matokeo makubwa sasa yaani the big resurts now huenda
mpango huo usizae matunda kutokana na changamoto zinazokabili sekta ya elimu wilayani Karagwe mkoani Kagera.



Hayo yalisemwa na wadau mbali mbali wa elimu wakati walipokuwa katika majadiliano katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika kiwilaya katika kata ya Kituntu wilayani humo hapo jana ambapo kwa upande wa wilaya ya Karagwe walipanga kuhitimisha siku hiyo April 08 mwaka huu.

Afisa elimu shule za msingi wilayani Karagwe Gidioni Mwesiga akiwa katika maadhimisho hayo alisema kuwa, ili kuhamasisha walimu juu ya mpango wa matokeo makubwa sasa watazunguka katika shule zote za msingi wilayani humo wakitoa mafunzo juu ya mpango huo na umuhimu wake.

Akiongea na gazeti hili Gidion Mwesiga ambaye  ni Afisa elimu shule za msingi wilayani humo alisema, kuna changamoto ya uhaba wa walimu ambapo halmashauri ya wilaya ya karagwe inahitaji walimu 1929.

Mwesiga alisema kuwa,wanao upungufu wa walimu 628 uwiano kwa mwalimu mmoja anafundisha wanafunzi 62 na  serikali kwa mwaka huu ilituma walimu 157 wakiripoti watakuwa na upungufu wa walimu 471.

Aliongeza kuwa changamoto hizo wao kama uongozi watazijadili na walimu, wanafunzi na wazazi ili ziweze kutatuliwa na hatimaye kuwa na wanafunzi wanaopata elimu bora wilayani humo na si bora elimu.

Vile vile alizitaja changamoto mbali mbali zinazokabili elimu katika wilaya yake kuwa ni pamoja na shule kutokaguliwa kwa wakati kutokana na ofisi ya ukaguzi kutokuwa na fedha ambapo kushindwa kukaguliwa kwa shule kunasababisha kutokuwa na kipimo bora juu ya elimu.

Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni kupata fedha kidogo ya ruzuku ya uendeshaji wa shule 
(capitation grant), fedha ambayo haikidhi mahitaji ya shule.



No comments:

Post a Comment