![]() |
maskini kitoweoo...!!!!!! |
Ng’ombe wapatao sita{5} wamefariki hapo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya kiasi kilichompelekea
kuchinjwa baada ya kupigwa na Radi iliyo piga mnamo saa moja na nusu asubuhi ya leo. Radi hiyo ilipiga baada ya mvua kubwa kuanza kunyesha na kusababisha vifo vyang’ombe hao mali ya Bw, MURISHIDI ABDALLAH maarufu kama {SHIIDI}, mkazi wa kijiji magata wilaya muleba. Wakiongea na Radio Karagwe wachungaji wan g;ombe hao wamesema kuwa wakati mvua inanyesha wao walikuwa wanataka kuanza kukamua maziwa na mvua ilipozidi waliondoka zizini hapo nakuingia kwenye nyumba wanamoishi, gaflandipo waliposikia kishindo kikubwa cha radi nakuanza kuona moshi ukitokea zizini. Aidha mmiliki wan g’ombe hao ndg; Murishidi amesema kuwa zizi lake lilikuwa na jumla ya ng’ombe 59 na walio fariki ni watano na mmoja kachinjwa, ameongeza kuwa hili swala yeye analichukulia kama changamoto na kusema kuwa hizi ni kadari za M/mungu kwani yeye ndiye aliempatia ng’ombe hao na pia yeye ndo kaamua kuwapeleka, lakini pia kamshukuru M/mungu kuwa hakuna binadamu aliyedhulika na tatizo hilo. Sanjari na hayo amevitaja vitu vingine vilivyo haribika kuwa ni pamoja na migomba kumi ambayo iko klaribu na zizi pamoja na uzio unaozungukuia zizi hilo.
Imetumwa na: ALLAWI BASHIRU {DJ KABAYSER}
No comments:
Post a Comment