CCM - MULEBA:
Kamati ya Siasa ya Wilayani Muleba imemaliza ziara yake ya siku mbili kwa
kutembelea miradi ya
maendeleo chini ya m/kiti wa {ccm} wilaya Ndg.
Muhhaji Bushako.
Ziara hiyo ilianzia katika kituo cha afya kaigara ambapo taarifa fupi
ilisomwa juu ya ujenzi wa world. Akisoma taarifa hiyo mbele ya viongozi
hao akiwemo mkuu wa wilaya muleba canal lemblesi kipuyo, mganga mfawidhi
wa kituo hicho alisema ujenzi huo ulianza tarehe 25/06/2013 na
kutarajia kukamilika may mwaka huu ambapo ujenzi wa world hiyo
umeghalimu jumla ya tsh.94,173,800/=.
Pamoja na changamoto zinazokikabiri kituo hicho ni pamoja na ukosefu wa
maji ambapo muhandisi wa maji ameonekana kutojali swala hilo.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na viongozi hao ni kituo cha afya
Kaigara, chanzo cha maji Katoke pamoja na tank la maji izigo,kituo cha
afya Izigo,ukaguzi wa barabara Izigo to Kyamkwikwi,ujenzi wa bweni
Rutabo sekondary, ukaguzi wa mladi wa maji kiota likiwemo tank la maji
na mladi wa umwagiliaji, ukaguzi wa ujenzi wa mnada wa mifugo Kyamyolwa,
mladi wa maji kabala pamoja na tank la maji, mladi wa maji nshamba na
mladi wa umwagiliaji Buhangaza.
Miladi yote iliyotembelewa miradi miwili ndio imekamilika na kukabidhiwa
kwa wakati, na miradi mingine kuwa na maswali ya sintofahamu lini
itakamilika na kuanza kutumika.
Aidha mkuu wa wilaya hiyo amewalalamikia wakuu wa idara husika kuwa
hawasimamii miradi hiyo kwa ufasaha na kuahidi kuwachukulia hatua za
kisheria juu ya ucheleweshaji wa mradi hiyo kwasababu zisizo za msingi.
Sanjari na hayo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauli ya Wilaya Muleba
Bi.ORIVA VAVUNGE atuhumiwa na wananchi wa kata Nshamba kuwa wizi wa
mashine za kusukuma maji na uharibifu wa chanzo cha maji Nshamba chanzo
ni yeye ambapo mabilioni ya fedha za Serikari zilitolewa kununua mashine
imara na badala yake zikafungwa mashine feki na hela kuliwa.
Wakiongea na Radio Karagwe kwa nyakati tofauti wa kijiji hicho ambao
pia ndo walengwa wa mladi huo akiwemo m/kiti wa NCCR wilaya muleba
Bw.Phagency Kapia wamesema kuwa chanzo cha matatizo yote na kutomalizika
miradi ndani ya wilaya ni Mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo.
Akihitimisha ziara hiyo mkuu wa msafara M/kiti wa {CCM} Wilaya Ndg
Muhhaji amewataka wkuu wa idara chini ya mkurugenzi wao na mkuu wa
wilaya kufanya kazi kwa uzalendo kama watanzania na kumalizia kuwa
kutomalizika kwa miladi kwa wakati ni swala lilomuumiza sana na kuongeza
kuwa hatua kali dhidi ya wakuu wa idara ambao hawafai hakuna sababu ya
kuendelea kuwakumbatia.
Imetumwa na ALLAWI BASHIRU……………
No comments:
Post a Comment